KUJINASUA KATIKA ROHO YA ADUI

| Makala

Katika ulimwengu wa Roho kuna mambo yanayoendelea na kutendeka ambayo yanabeba hatma za maisha yetu na sisi hatujui wala kufahamu,

Kila kitu huanzia rohoni, maana hata mwanadamu wa kwanza alianzia rohoni kisha mwilini, yapo mambo unayoyaona na usiyoyaona kwa macho ya nyama, yameanzia rohoni na yamebaki rohoni ila mengine yamefunuliwa nasi tunayaona.

Hatma za maisha yetu sisi sote zinaamuliwa na maamuzi yanayofanyika rohoni,

Wewe kukubalika ama kukataliwa,kushinda au kushindwa,kuendelea ama kukwama, chanzo kipo rohoni.

Anaandika kwenye kitabu cha Yohana {3} sura ya kwanza na mstari wa pili, anasema “Mpenzi naomba ufanikiwe na kuwa na afya yako kama vile ROHO yako ifanikiwavyo.

Kila shida na changamoto ambayo unakutana nayo na inakutesa kwenye maisha yako ina sababu na chanzo chake, ndiyo maana tunasisitiza wakati wote usichukulie kawaida maisha,yatazame kwa jicho la tatu la kiroho na uyapime yana mpango upi kwa upande wako…

Vitu kama:

Biashara isiyo na faida nk……

Malezi ya mzazi mmoja

Talaka

Ndoto mbaya

Kujichua

Uzinzi

Madeni

Umasikini

Magonjwa

 

Suala la kuwa connected na uharibifu wa adui linawafikia wanadamu kwa njia kuu mbili:

Kuna njia ya kutakiwa na watu,

na njia ya kujitakia wenyewe.

Tutaendelea zaidi sehemu inayofuata….

Pastor Innocent Mashauri

Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA

Maarifa ya kiMungu

+255 758 708 804


 SADAKA